#SalamaNa #SendTip Through MPESA #5578460
Nikuibie tu siri ya kabatini kuhusu haya mazungumzo yangu na Aunty Ezekiel, kwanza ilikua ngumu sana mpaka alipofika hapa kwenye kiti maana mazungumzo haya yalighairishwa zaidi ya mara tatu mpaka ilipofika siku hii. Kwa imani yangu nisema Mungu ana mipango yake, yaani kila kitu kwa wakati wake na bila ya shaka wakati wa hii ulikua haijafika bado ndo maana haikutokea na kwa kutokea siku hii, huu ndo ulikua wakati sahihi kabisa.
Mimi na yeye tunafahamia ki vyetu, si watu ambao tunakutana kila siku ila ni watu ambao tukikutana tuna click tu vizuri na mambo yanaenda. Marafiki zetu wengi pia wanafahamiana kwahiyo tunaenda tu vizuri. Na nia na madhumuni ya sisi kumtaka kwenye kiti chetu ni kwasababu wote tunajua amepitia mengi na kwa yeye kutusimulia kuhusu makuzi yake na mahangaiko yake yanafaa nafasi kwenye kiti chetu.
Toka mara ya kwanza kusikia jina la Aunty Ezekiel naamini miaka mingi tu ishapita, kama wewe ni wale wa zamani kama mimi basi utakua unamjua toka miaka ya katikati ya 2000 baada ya kuwa mmoja ya kundi la wasichana wazuri ambao walishawahi kushiriki Miss Tanzania. Kwenye mwaka ambao Aunty alishiriki kulikua na warembo kama Wema Sepetu, Jokate Mwegelo na Irene Uwoya kuwataja tu wachache. Aunty yeye naye alikua kati ya wale waliongia Top 10. Mwaka huo ulikua mwaka wa ushindani sana lakini wengi ambao walimaliza vizuri ndio hawa mpaka leo wanaendelea kufanya vizuri katika nyanja mbali mbali ambazo wao wamezishagua.
Aunty sasa ni Mama wa watoto wawili ambao ameniambia ni kila kitu kwake, wanampa sababu ya kutaka kuendelea kuishi na kuwa bora kwao kila wakati, nilimuuliza siku ya kwanza alipompata mtoto wake wa kwanza, na hisia yake ilikuaje, na anakumbuka jinsi ambavyo aligundua ana ujauzito na mara ya kwanza anamshika Cookie mikononi mwake.
Aunty pia anakumbuka ‘ujana’ wake na mengi aloyapitia mpaka akawa hivi alivyo leo.
Kuna suala la yeye kuwa na mahusiano na wanaume ambao ni wadogo kuliko yeye, au wale ambao alikua nao zamani ambao walikua wakubwa kuliko yeye, Aunty amenielezea maoni yake juu ya hili. Mahusiano yake na Marehemu Mzee wake, Mama yake.. Alivyolelewa na machaguzi ambayo aliwahi kuyafanya wakati anakua na pengine maamuzi mabaya au kama ana majuto katika maisha yake.
Kama binadamu kuna baadhi ya mambo yanakua magumu kuwa nayo wazi au kuyaelezea kinaga ubaga, Ila hata kwa haya ambayo tuliongea nae natumai utapata ya kujifunza kupitia yeye.
Tafadhali Enjoy.
Love,
Salama.
Support us through https://anchor.fm/yahstonetown/support
SUBSRIBE TO OUR CHANNEL https://bit.ly/YahStoneTownSubs
Listen our Podcast on
Spotify Link https://spoti.fi/2Uxr6Cm
ApplePodcast Link https://apple.co/2Ou1bru
GooglePodcast Link https://bit.ly/GooglePodcastSalamaNa
Audiomack Link https://bit.ly/YahStoneTownAudioMack
YouTube Link http://bit.ly/YoutubeSalamaNa
Soundtrack Yeah by @MarcoChali https://www.youtube.com/watch?v=Cue1HB4fnLQ
Follow:
Twitter: http://twitter.com/YahStoneTown
Instagram: http://Instagram.com/YahStoneTown
Facebook: http://facebook.com/YahStoneTown
Channel Administered by Slide Digital
Instagram: www.instagram.com/slidedigitaltz