Rais John Magufuli ametembelea wilaya ya Bariadi jimboni kwa mbunge Andrew Chenge na kuweka jiwe la msingi la mradi mkubwa wa maji wa Lamadi sambamba na kufungua barabara za Mji wa Lamadi katika Wilaya ya Busega.
Pia katika ziara hiyo Rais Magufuli amefungua jengo la wagonjwa wa nje (OPD) la Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu, na ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa kiwango cha lami wa barabara ya Maswa – Bariadi.
Rais Magufuli alikaribishwa na mkuu wa mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka ambaye pia alimmwagia sifa za kuwa Mkuu wa Mkoa bora zaidi miongoni mwa wakuu wa mikoa wote kiutendaji.
Hii hapa hotuba yake nzima aliyoitoa kwa wananchi wa Bariadi na taifa zima.