MENU

Fun & Interesting

Jaji Warioba ataja mambo manne yazingatiwe Katiba Mpya

Mwananchi Digital 6,046 11 months ago
Video Not Working? Fix It Now

Kampuni ya Mwananchi Communications LTD wasambazaji wa magazeti ya Mwananchi, Thecitizen na Mwanaspoti Tanzania. Joto la mchakato wa Katiba mpya halijapoa baada ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba kusisitiza: “Mjadala na mashauriano juu ya Katiba mpya unapaswa kuendelea hadi 2025.” Jaji Warioba amebainisha maeneo makuu manne yanayopaswa kupata mwafaka wa kitaifa kabla ya kwenda kwenye kura ya maoni ya Katiba Pendekezwa ni suala la maadili, madaraka ya Rais, mambo ya uchaguzi na muundo wa Muungano. Amesema mambo hayo yasipopata mwafaka itakuwa vigumu kwa Katiba Pendekezwa kuridhiwa na wananchi.

Comment