Kuku wa kienyeji huwa nachukua muda wa miezi 7-8 kuanzia vifaranga mpaka kuanza kutaga.
kwenye Makala ya leo tutajifunza jinsi ya kuwalisha kuku wa kienyeji ili wakuwe haraka, wawe na afya njema na waanze kutaga mapema.
Kinacho sababisha vifaranga wa kienyeji kushambuliwa na magonjwa yanayosababisha vifo ni lishe duni, mazingira machafu na baridi.
Tukianza na swala la Lishe, kuku kama walivyo viumbe wengine wanahitaji kupewa chakula chenye virutubisho vyote muhimu ili wakuwe hara na wawe na afya njema, virutubisho hivyo ni:-
Wanga ili kuupa mwili nguvu
Protein ili kujenga mwili
Mafuta ili kuupa mwili joto
Vitamin ili kuulinda mwili dhidi ya magonjwa
Madini ili kuimarisha misuli, mifupa na ganda la yai
Maji safi ili kusafirisha virutubisho vingine na kuufanya mwili uwe hydrated
Kifaranga akipata virutubisho vyote hivyo utamuepusha na stress hivyo atakuwa kwa haraka na kufikia uzalishaji wa nyama na mayai.
Chakula cha kuku kimeganyika kwenye makundi matatu kulingana na umri na uhitaji wa Protini mwilini.
Umri wa siku 1 - Wiki 8 walishe Chick stater/mash
Umri wa wiki 9 - 18 walishe grower mash
Umri wa wiki 19 na kuendelea walishe layer mash
Ukiwalisha vifaranga wa kienyeji chakula cha dukani kwa muda wote, hautaiona faida ya ufugaji na kwakuwa kuku wa kienyeji wanauwezo mkubwa wa kujitafutia chakula na pia uwezo mkubwa wa kumeng'enya virutubisho vinavyopatikana kwenye mabaki ya chakula cha nyumbani na shambani., Nakushauri uwalishe vifaranga wa kienyeji kama ifatavyo:-
Miezi 2 ya mwanzo walishe chick stater/mash
Na baada ya hapo wachanganyie concentrate na pumba kwa kufata maelekezo ya mtengenezaji.
Concentrate ni chakula kilichochanganywa kwa virutubisho vyote muhimu lakini vipo kwa kiwango kikubwa, ili kuweka uwiano sawa wa hivyo virutubisho unatakiwa kuchanganya na pumba.
Sasa kumekuwa kunachangamoto ya stater ya aina gani itumike.
Kwa uzoefu nilionao kwenye ufugaji wa kuku, vifaranga wakipewa stater ya unga wanakula kwa kuchambua punjepunje pekee, hawana muda na ule unga hivyo wanabakisha virutubisho vingine muhimu.
Ndio maana unaweza kuwapa chakula bora lakini vifaranga wakaendelea kudumaa, na kukosa nguvu za miguu.
Nikushauri sasa ubadilishe chakula unachowapa vifaranga, wape stater ya pillet.
Pillet ni chakula ambacho kiko katika mfumo wa punjepunje hivyo kuku watakula virutubisho vyote bila kubakisha chochote.
Kwa siku ya 1-21 Nakushauri uwape bila kuwapimia na kuanzia siku ya 22 anza kuwapimia kwa utaratibu unaouona kwenye screen.