MENU

Fun & Interesting

JUMA NATURE | THE LEGEND SHOW EPISODE 6

Bongo Records Ltd 18,000 2 months ago
Video Not Working? Fix It Now

Wilaya ya Temeke inajulikana tangu kitambo kuwa na wanamuziki wakali sana na waasisi baadhi wa muziki wa kizazi kipya walitokea huko. Wasanii kama Chief Ramso (Zavara) kinara wa pioneers Kwanza Unit alitokea Temeke, lakini pia kulikuwa na GWM, N2P, LWP na Inspekta Harun. Lakini aliposikika tu kwa mara ya kwanza SIR NATURE basi hadithi ya ufalme wa Temeke ikabadilika na Nature akatajwa kama mfalme wa TMK. Alijaaliwa kipaji cha kurap na kuimba ambavyo si rahisi sana kwa kila mwanamuziki na ukali wake ulifanya ashirikishwe na wasanii wengi sana mahiri kama Profesa Jay, Mabaga Fresh, Ferooz, Solo Thang, GWM, Soggy Doggy, Rich One na wengi mtakumbuka alivyopanda stejini kwenye tamasha la Fiesta kufanya show na mwanamama Lil Kim kutoka Marekani na akaacha historia. Juma Nature aliweka pia rekodi ya kuujaza ukumbi wa Diamond Jubilee akizindua album yake ya Ugali na hata ungewauliza wauzaji wa albums kipindi kile wangekwambia Juma Nature alikuwa ndani ya "Top 10" ya wanamuziki waliouza zaidi kazi zao.

Comment