MENU

Fun & Interesting

KIMEUMANA! WANACHAMA 20 WA CHADEMA WAKAMATWA WAKIFUATILIA SAKATA LA MWENZAO ALIYETOWEKA

Mwananchi Digital 8,063 lượt xem 23 hours ago
Video Not Working? Fix It Now

Wanachama na viongozi 20 wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Kanda ya Viktoria wamekamatwa na Polisi wakiwa njiani kwenda kuonana na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Said Mtanda.

Makada hao akiwemo Katibu wa Chadema Kanda ya Viktoria, Zakaria Obadi na wenzake wamekamatwa leo Jumatano, Februari 26, 2025 nje ya ofisi za mkuu wa mkoa na kuwekwa mahabusu kwa dakika kadhaa kisha kuachiwa kwa dhamana.

Habari za kuaminika zinaeleza kuwa makada na viongozi hao walikuwa kwenye harakati za kumuona Mtanda ili kufahamu hatima ya Katibu wa Baraza la Vijana wa chama hicho (Bavicha) Mkoa wa Mwanza, Amani Manengelo aliyetoweka tangu Februari 14, 2025 akiwa wilayani Misungwi.

Akizungumzia kukamatwa kwa makada hao, Mjumbe wa Kamati Kuu Chadema, Salma Kasanzu amesema wanachama hao walikuwa sehemu ya ujumbe wa ufuatiliaji alipo Manengelo na walikwenda kumuona Mtanda, lakini wakakamatwa kabla ya kumuona bila kuelezwa sababu.

Soma kwa undani katika Tovuti ya Mwananchi.

Imeandikwa na Damian Masyenene

Comment