Ni takribani watu 4 tu kati ya 10 huweka malengo yao ya mwaka. Na kati yao hao wanne (4) ni asilimia 8% tu huweza kuyafikia malengo hao.
Timiza Malengo Yako kwa kuzijua siri, tabia na sifa walizonazo wale wenye kufanikisha malengo yao.
Hatua ya muhimu sana ni kuamua kuwa na malengo ya mwaka. Hatua inayofuata ni kuyafanyia kazi hayo malengo.
Hata hivyo, kuwa na malengo peke yake haitoshi; bado unaweza kushindwa kuyafikia malengo hayo (kama ilivyo kwa 92%).
Fahamu mambo ambayo hufanywa na 8% ya watu wanaoweka malengo yao ya mwaka ambayo 92% walioshindwa hawayafanyi. Mambo hayo ni:
1. Kuwa tayari kubadilika - ili kupata matokeo ya tofauti
2. Kuwa na picha (maono) ya matokeo wanayoyatafuta
3. Kuwa na orodha iliyoandikwa ya malengo yao (kwa wakati)
4. Kugawa malengo kwenye hatua ndogondogo
5. Kukamilisha lengo (hatua) moja kabla ya kuendea na lengo/hatua nyingine
6. Kuomba msaada pale wanapouhitaji
7. kushirikiana na watu wenye mtazamo na malengo yanayoendana na ya kwao
Jifunze zaidi na Michael Kamukulu kupitia LENZI @lenzi.michaelkamukulu
#malengo #mafanikio #2024 #chaguamwenyeweleo #2023 #lenzi #michaelkamukulu
Chapters
00:00 Wachache wanaweka na kufanikisha malengo
00:41 Kwa nini tunaweka malengo?
01:53 Kwa nini wengi hawatimizi malengo
03:06 1. Kuongozwa na picha (maono) ya matokeo
04:49 2. Kuandika Orodha ya Malengo
06:24 3. Kugawa malengo katika hatua
08:01 4. Kukamilisha hatua moja kwa wakati
08:39 5. Kupumzika na Kujitathmini
10:10 6. Kuomba Msaada