Kuku kama wanyama wengine hushambuliwa na magonjwa mbalimbali ambayo mengine yanatibika kwa dawa na mengine hayana tiba bali kuku hupewa chanjo maalumu ili kuzuia magonjwa hayo.
Leo nitawaeleza baadhi ya magonjwa ambayo hushambulia kuku mara kwa mara na ambayo ni chanzo cha kuwakatisha tamaa wafugaji wa kuku
Magonjwa ndio husababisha hasara katika ufugaji wa kuku. Kuku waliochanjwa dhidi ya magonjwa hudumisha afya bora. Jaribu kila mara kuzuia magonjwa, kwani kuzuia ni bora kuliko kuponya. Kinga yaweza kutolewa mara kwa mara (kila baada ya miezi mitatu)