Magonjwa ya Vifaranga vya Kuku wa Kienyeji ni changamoto kubwa kwenye ufugaji wa kuku ambayo huwakatisha tamaa Wafugaji wengi kwa sababu ya vifo vingi hasa kipindi cha uleaji wa vifaranga vya kukuwakienyeji.
Magonjwa yamegawanyika katika makundi mbalimbali kulingana na wadudu wanaosababisha magonjwa hayo.
Kuna magonjwa yanayo sababishwa na virusi, magonjwa yanayo sababishwa na bakteria, magonjwa yanayo sababishwa na protozoa, magonjwa ya upungufu wa lishe na magonjwa yanayosababishwa na wadudu (minyoo, viroboto na utitiri).
Bakteria wanaosababisha magonjwa ya vifaranga vya kuku wa kienyeji hupatikana kwenye miili ya kuku wagonjwa, utumbo, makamasi, na vinyesi vyao.
Aidha, katika mazingira machafu na vyakula, maji, hewa, na vifaa vya kazi vilivyo chafuliwa.
Mazingira yenye unyevunyevu na joto ni vichocheo vya kuzaliana na kusambaa kwa hao bakteria.
Magonjwa ambayo yameelezewa kwenye video hii ni
1. Typhoid
2. Kipindupindu
3. Coccidiosis
Sasa kwakuwa magonjwa yote yamebainika kwenye banda moja sasa unapaswa kutumia dawa yenyeuwezo wa kutibu magonjwa yote, mfano wa dawa hiyo ni ESB3 30% n.k Au
Uchanganye dawa zifatazo Trisulmycine na Amprollium.
Kwa Magonjwa ya Upungufu wa Lishe, hakuna tiba zaidi ya kuwapa lishe inayotakiwa kwa kipindi chote cha ukuaji wao
SUBSCRIBE: https://bit.ly/2OvSiRm
PLAYLIST
Ufugaji wa Kuku wa Kienyeji
https://goo.gl/2Wkyhc
Magonjwa ya Kuku
Bofya link kutazama video hizo
https://goo.gl/hvfVcg
Uleaji wa vifaranga vya kuku Kwa Kutumia Brooder
https://goo.gl/xSTCfX
Instagram
www.instagram.com/Changamkiafursatv
What's spp
+255752209073