MENU

Fun & Interesting

Mambo 5 Yanayokupoteza Kwenye Ramani | Michael Kamukulu

LENZI Mindset | Michael Kamukulu 1,273 lượt xem 6 days ago
Video Not Working? Fix It Now

Sio kila anayefanya jambo jema anaishia kupata matokeo mazuri. Na hata akiyapata matokeo anayotafuta, kuna uwezekano wakanufaika wengine zaidi yake. Maisha ya kila mtu yanayo ramani; usipojua kuisoma vema unaweza kupotea na kupoteza ndoto na mafanikio yako kwa urahisi. Ukikimbiza kila kitu, utapoteza kila kitu. Kwa hiyo, chagua njia yako kwa makini sana ili usije ukaishia kuumia au kuumizwa.

Katika video hii, tunakuelezea kwa undani kuhusu Njia 5 Rahisi ambazo zinaweza kukusaidia Kupotea Kwenye Ramani yako ya maisha.Ungana na Michael Kamukulu kupitia @lenzi.michaelkamukulu ili uweze kujifunza kwa kina zaidi.

Tunaziangalia njia tano rahisi ambazo zinaweza kukupotosha kwenye mapambani ya kutafuta hatua za mafanikio. Hizi ni tabia ambazo zinaweza kukufanya upoteze mwelekeo wako na malengo yako kwa sababu unaweka nguvu kubwa kwenye kujali na kutimiza matarajio ya wengine badala ya kulinda, kupambana na kuzitafuta ndoto zako binafsi.

Njia tano tgunaziongelea ni hizi hapa:

1. Kuwa Mkombozi wa Ukoo
Kujitolea sana ili kuokoa familia au ukoo kunaweza kukufanya usahau kujali maendeleo yako binafsi. Kuwa mkombozi wa ukoo ni jukumu kubwa ambalo linaweza kukufanya usahau malengo yako binafsi na kukuweka katika nafasi ya kuendelea kusaidia wengine badala ya kujiajali.

2. Kusaidia Kila Mtu
Kuwa na moyo wa kusaidia ni sifa njema, lakini kujihusisha na kila changamoto ya watu wote kunaweza kukufanya upoteze muda na nguvu zako. Ni muhimu kuweka mipaka ili kuweza kujikita katika mambo ambayo yanaongeza thamani katika maisha yako.

3. Kuweka Kipato Chako Wazi kwa Kila Mtu
Siri na usimamizi wa fedha ni muhimu kwa mafanikio ya kibinafsi. Kuweka kipato chako wazi kwa kila mtu kunaweza kusababisha matatizo ya usimamizi wa fedha na kuongeza matarajio yasiyofaa kutoka kwa wengine, jambo ambalo linaweza kukupotosha katika maamuzi yako ya kifedha.

4. Kumridhisha Kila Mtu
Kutaka kuwafurahisha kila mtu ni mzigo mkubwa unaoweza kukufanya usahisi na kupoteza utambulisho wako. Ni muhimu kuelewa kuwa sio kila mtu atakubaliana na maamuzi yako; jifunze kuwa mwaminifu na usikubali maoni ya kila mtu kuwa kizuizi katika maendeleo yako.

5. Kutembea na Kila Trend (Msimu)
Kufuata kila mtindo unaotokea bila kufikiri kina kunaweza kukufanya upoteze msingi wa malengo yako. Badala ya kuruka kwenye kila trend, chagua zile ambazo zinaendana na maadili yako na malengo yako halisi, ili usiwe mkimbia kila kitu kinachopita kwenye mtandao.

Kumbuka, ni muhimu kuchukua muda wa kujitathmini na kuelewa ni wapi unapaswa kuweka mkazo ili usiruhusu mawazo na tabia za wengine zikuelekeze mbali na ndoto zako. Chagua njia yako kwa busara na uendelee kujifunza ili kufikia mafanikio unayoyataka.

———————————————
Wasiliana nasi kwa huduma zaidi ikiwemo:

1. Mafunzo na mwongozo maalum wa kufikia malengo (personal/individual coaching)
2. Mafunzo na mwongozo maalum kwa makundi na taasisi (group coaching)
3. Ushauri wa kitaalam kuhusu maendeleo binafsi (personal development)

Mawasiliano yetu:
Simu: +255 752 465 039
Baruapepe: lenzimindset@gmail.com

* * *

Pata Kozi Kuhusu jinsi ya kujiajiri na kuongeza kipato kwa kutumia MAUDHUI kwa bei nafuu ya TZS 15,000 tu kupitia hapa https://tr.ee/UTrb-ghbfk

#HatuaMojaMbeleKilaSiku #michaelkamukulu #lenzimindset #lenziacademy

* * *

Chapters
00:00 kupotea kwenye ramani
00:16 1. Mkombozi wa Ukoo
02:23 2. Kusaidia Kila Mtu
04:04 3. Kuweka wazi Kipato Chako
05:16 4. Kumridhisha Kila Mtu
06:08 5. Kutembea na Trend (Msimu)
07:05 Closing

Comment