MENU

Fun & Interesting

MAPYA VITA M23, FARDC, AFRIKA KUSINI YAMWAGA WANAJESHI NCHINI CONGO

Mwananchi Digital 41,749 2 weeks ago
Video Not Working? Fix It Now

Afrika Kusini imetuma wanajeshi wa ziada na vifaa vya kijeshi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), ili kukiongezea nguvu kikosi cha Ulinzi wa Amani cha Umoja wa Mataifa (Monusco) kilivyoko nchini humo. Shirika la Habari la Reuters limeripoti jana kuwa uamuzi wa Afrika Kusini kupeleka wanajeshi wa ziada umefanyika zikiwa zimepita siku 19 tangu Waasi wa M23 waiteke miji ya Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC). Vyanzo vya vyanzo vya kisiasa na kidiplomasia vimesema, uamuzi huo umechukuliwa baada ya wanajeshi wake 14 kuuawa katika mapigano na waasi wanaoungwa mkono na waasi hao wanaodaiwa kufadhiriwa na Rwanda. Hata hivyo, katika mahojiano yake na CNN, Rais wa Rwanda, Paul Kagame alikanusha kuifadhiri M23, huku akisema hafahamu kama kuna wanajeshi wa Jeshi la Ulinzi la Rwanda (RDF) wako nchini DRC. Kuimarishwa kwa kikosi cha Afrika Kusini kunakuja wakati wa hofu kwamba mapigano mashariki mwa DRC yanaweza kuchochea vita ya kikanda eneo lenye mzozo huo wa muda mrefu, ambalo kwa miongo mitatu iliyopita limekumbwa na mauaji ya raia, migogoro ya mipakani, na uasi wa mara kwa mara. Takwimu za safari za ndege zilizopitiwa na Reuters zilionyesha kuwa ndege za usafirishaji zilisafiri kutoka Afrika Kusini hadi Lubumbashi, kusini mwa DRC. Mfanyakazi mmoja wa uwanja wa ndege mjini Lubumbashi aliithibitishia Reuters kuwa ndege za kijeshi zilikuwa zimetua wiki iliyopita. “Tumejulishwa kuhusu kuongezeka kwa wanajeshi wa (Jeshi la Ulinzi la Afrika Kusini - SANDF) katika eneo la Lubumbashi. Tunakadiria kuwa takriban wanajeshi 700-800 wamepelekwa huko,” Mbunge wa Afrika Kusini, Chris Hattingh, aliiandikia Reuters. Imeandikwa na Mgongo Kaitira kwa msaada wa Mashirika.

Comment