MENU

Fun & Interesting

Salama Na MAJIZZO SE6 EP17 | MPIMAJI PART 1| SendTip MPESA LIPA NO 5578460

YahStoneTown 135,410 3 years ago
Video Not Working? Fix It Now

#SalamaNa #SendTip Through MPESA #5578460 MPIMAJI Francis Ciza that’s the name, anastahili heshima yake kwa ujasiri mkubwa ambao ameuonyesha kabla hajafika hapa alipo leo. Njia yake kwa mujibu wa haya maongezi yetu ilikua ya kulazimisha sana na yeye hakuwahi kukata tamaa, au tuseme neno au wazo la kukata tamaa halijawahi kuwa mawazoni mwake. Majay ndo jina la umaarufu wake, Dj Majay au RDJ Majay au Majizzo moja ya ma Dj walokua wakiunda kundi la ‘Kwa Fujo DJ’s’ akiwa pamoja na Abubakar Sadique na ma Dj wengine wakati huo. Jinsi gani walikutana na nini kiliwafanya wawe na umoja huo? Tulimuuliza Majay kwenye maongezi haya na akaniambia waliona kitu ambacho hakuna mtu mwengine alikiona wakati huo na kweli kilifanya kazi. Nini sasa kilisababisha umoja wao kuvunjika? Nini special kwake ambacho anadhani kinamfanya aendelee kuwa mwenye mafanikio na relevant kuliko wenzake? Huku sasa anatuelezea rasilimali yake aliyopewa na Mwenyezi Mungu, ya KUTOKATA TAMAA. Ambayo ndo imemfanya yeye anendelee kubaki kuwa nahodha wa boti yake ambayo imeweza kupambana na dhurba nyingi za baharini na nchi kavu lakini bado inaendelea na safari. Majay alianza kutafuta kwake kama fundi nguo, wengi tunawaita fundi cherehani, anatuambia mtaani kwake kulikua na MC mmoja wa harusi ambaye yeye ndo alikua anamshonea nguo zake na siku ambayo alimchukua Majay kwenye moja ya kazi zake ndo siku ambayo maisha ya Majay YALIBADILIKA. Sasa ni CEO wa moja ya Radio zenye nguvu hapa Tanzania na mpambanaji ambaye anahakikisha vijana na mziki wetu wa kizazi kipya unazidi kwenda mbali, yeye ni mtu ambaye anawavutia vijana wengi kwa kuwapa matumaini kwamba kuna siku mazuri yatakuja tu, at least hiyo ndo vibe ambayo mimi naipata kwake. Ashakataliwa sana. Ashakosea sana, ashafungiwa milango sana, ashakimbiwa sana na marafiki ambao walikua hawaamini kwenye ndoto yake na amesha anza upya mara kadhaa kwa kuamini kwamba kama aliweza kukipata mwanzo, basi inawezekana kukipata tena, na hivyo ndo jinsi ambavyo ilikua na inaendelea kuwa mpaka leo hii. Kama unahitaji inspiration au mtu wa kumtazama ndoto zake ili na wewe uweze kuzitimiza za kwako basi Francis Ciza anaweza kukusadia sana. Tafadhali enjoy mazungumzo yetu haya ambayo yamejaa safari ndefu ya kuanzia kwenye kupima watu viuno na kifua mpaka kuwapangia watu burudani isiyochosha. Love, Salama. Support us through https://anchor.fm/yahstonetown/support SUBSRIBE TO OUR CHANNEL https://bit.ly/YahStoneTownSubs Listen our Podcast on Spotify Link https://spoti.fi/2Uxr6Cm‬ ‪ApplePodcast Link https://apple.co/2Ou1bru‬ GooglePodcast Link https://bit.ly/GooglePodcastSalamaNa Audiomack Link https://bit.ly/YahStoneTownAudioMack ‪YouTube Link http://bit.ly/YoutubeSalamaNa Soundtrack Yeah by @MarcoChali https://www.youtube.com/watch?v=Cue1HB4fnLQ Follow: Twitter: http://twitter.com/YahStoneTown Instagram: http://Instagram.com/YahStoneTown Facebook: http://facebook.com/YahStoneTown Channel Administered by Slide Digital Instagram: www.instagram.com/slidedigitaltz

Comment