Nilikua nimepumzika sebuleni nikitizama vipindi mbalimbali vya kwenye Runinga nikiwa pamoja na dada wa kazi aitwae Kalunde.
Punde baba alirejea kutoka kazini huku akiwa na mtu ambae sikua nikimfahamu.Alikua ni kijana mmoja hivi mwenye mwili uliojengeka vyema kwa misuli tena akionekana ni mkakamavu hasa.