MENU

Fun & Interesting

SHAHIDI AIELEZA MAHAKAMA ALIVYOONA VIUNGO VINAVYOFANANA NA MAUMBILE YA KIKE

Mwananchi Digital 2,078 1 day ago
Video Not Working? Fix It Now

Mashahidi wa Upande wa Jamhuri katika kesi ya mauaji ya kukusudia inayomkabili, Josephine Mngara (30), aliyeuawa kwa kuteketezwa kwa moto, wameieleza Mahakama namna walivyobaini uwepo wa mabaki ya mwanadamu. Mbali na mashahidi hao, daktari aliyeuchunguza mwili huo, ameeleza ulikuwa ni mkaa isipokuwa sehemu ya nyuma ya kichwa, mapafu na moyo, misuli ya makalio na sehemu ya nyonga ambayo ilionyesha sehemu ya siri ya jinsia ya kike. Kesi hiyo ilianza kusikilizwa jana Jumatatu, Februari 24, 2025 mbele ya Jaji Adrian Kilimi wa Mahakama Kuu Kanda ya Moshi, huku upande wa mashitaka ukiongozwa na Wakili Mwandamizi wa Serikali, Kambarage Samson, akishirikiana na Frank Ong'eng'a na Grace Kabu. Mbali na mawakili hao, lakini utetezi katika kesi ya mauaji namba 3382/2024, inayowakabili washtakiwa wawili, Erasto Mollel na Samwel Mchaki, unawakilishwa na mawakili wa kujitegemea, Alfredy Sindato Silayo na Lilian Mushi.

Comment