MZIZIMA DERBY | Ni sare ya 2-2 kati ya Simba SC dhidi ya Azam FC, mchezo wa ligi kuu ya NBC, uliopigwa kwenye Dimba la Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.
Azam wametangulia kwa goli la Gibril Sillah dakika ya 01, kabla ya Elie Mpanzu kusawazisha dakika ya 25 na Abdulrazak Hamza kuongeza la pili dakika ya 76.
Nyota wa mchezo ni ‘Super Sub’, Zidane Sereri ndiye aliyeweka mambo sawa kwa kuifungia Azam FC bao la kusawazisha dakika ya 88, kwa assist ya aina yake kutoka kwa Feisal Salum Feitoto.