MENU

Fun & Interesting

SWAHILI: Jinsi ya Kuzuia na Kusafisha Ukungu Nyumbani Mwako | Preventing & Cleaning Mold at Home

Video Not Working? Fix It Now

Ukungu ni aina ya Kuvu ambayo inaweza kukua mahali popote kuna unyevu, ikiwa ni pamoja na kwenye chakula, vifaa vya ujenzi, nguo na samani. Kukaa karibu na ukungu kunaweza kuathiri afya yako, kwa hiyo ni muhimu kuelewa jinsi ya kuiondoa. Ukungu unaweza kusababisha pumu, maumivu ya kichwa, uchovu, macho, ngozi kuwasha, mizio na zaidi. Uzoefu wa mwili wako kwa sababu ya ukungu hutegemea aina ya ukungu, kiasi cha ukungu, ni muda gani umekua karibu na ukungu, na afya yako kwa ujumla.Video hii itaanza kwa kushiriki vidokezo vya jumla vya kuzuia na kuondoa ukungu, na kisha tutazungumzia kuhusu kitu ambacho unahitaji kufanya, ikiwa mafuriko yanasababisha ukungu nyumbani kwako.Ikiwa unakodisha nyumba yako, zungumza na mwenye nyumba wako kuhusu matatizo ya ukungu. Ikiwa hatachukua hatua yeyote kushughulikia tatizo la ukungu, unaweza kuwasilisha malalamiko kwa Kitengo cha Usalama wa Moto.Ikiwa una maswali kuhusu haki zako, wajibu, au hali ya maisha kama mpangaji linalohusiana na suala la ukungu, kunao watu wa kukupa usadizi. Wapigie: Wapangaji wa Jimbo la Vermont kwa nambari (802) 864-0099 au, uwatumie barua pepe kwenye anwani hii ili kuzungumza na mtu anayeweza kukupa usaidizi. Kuna rasilimali zaidi kwenye tovuti hii: ili kuzuia ukuaji wa ukungu, kuhepuka kuweka maji ya ziada na unyevu nje ya nyumba yako, ni muhimu sana. Hakikisha umerekebisha paa zinazovuja, mifereji ya maji, madirisha na mabomba ili maji yasiingie. Ni muhimu pia kuweka maji mbali na msingi wa nyumba yako. Kwa swala la ndani ya nyumba, hakikisha kifaa chako cha kukausha nguo na feni za jikoni na bafuni zinasukuma hewa nje. Ikiwa nyumba yako ina unyevu mwingi, unaweza kununua mashine inayoitwa “De-hu-mid-ifier” ya kuvuta maji kutoka hewani, haswa katika maeneo yenye unyevu-nyevu kama orofa yako ya chini. De-hu-mid-ifier itaonyesha kiwango cha unyevu katika nyumba yako. Jaribu kuweka viwango vya unyevu kati ya asilimia 40 hadi 60. Hakikisha unatumia aina sahihi ya kiziba baridi au insulation katika nyumba yako ili kusaidia kuweka hali iwe kavu. Jinsi ya kuondoa UkunguUpimaji wa ukungu sio lazima au kupendekezwa. Majaribio au upimaji hauwezi kuonyesha kama jengo liko salama au si salama. Haijalishi ni kiasi gani au aina gani ya ukungu uko katika jengo lako, hata hivyo unachohitaji kufanya ni kile kile: ondoa vitu vyenye ukungu, kausha nafasi hio, na urekebishe tatizo la maji au unyevu.Kwa kawaida unaweza kusafisha ukungu wewe mwenyewe ikiwa eneo lenye ukungu liko ni chini ya futi 10 za mraba, au takriban mita tatu za mraba. Hakikisha unajilinda kwa kuvaa nguo zilizo na mikono mirefu, suruali ndefu, buti zilio kavu, kinga za mikono au glavu, miwani, na barakoa ya nambari N-95. Watoto na watu wazima wenye matatizo ya kupumua, na watu walio na kinga dhaifu, hawapaswi kuwepo wakati wa kusafisha ukungu. Tumia maji na sabuni kusafisha ukungu kwenye vitu ambavyo haviloweshi maji, kama vile plastiki au glasi. Tupa vifaa vinavyo fyonza maji kwa urahisi kama zulia.Osha nguo ambazo zimegusana na ukungu katika maji ya moto tofauti na nguo zingine.Baada ya kusafisha ukungu, fagia ukitumia ombwe kwenye nyuso zote kwa utupu wa HEPA.Aina hizi za vacuum zina vichungi vinavyo nasa chembe ndogo ndogo kama vumbi, poleni, ukungu na bakteria. Ili kuhakikisha kama utupu una kichujio cha HEPA, angalia mwongozo wa maagizo au tovuti ya mtengenezaji.Uondoaji wa Ukungu wa Kitaalamu Ikiwa ukungu hufunika eneo kubwa,zaidi ya futi 10 za mraba, ni vyema kumwita mkandarasi ambaye anajua jinsi ya kusafisha ukungu. Ikiwa unakodisha nyumba yako, au unafanya kazi katika jengo ambalo lina ukungu, zungumza na mwenye nyumba hio au mwajiri wako. Ikiwa tatizo la ukungu halita tatuliwa, wapangaji wanaweza kuwasilisha malala-miko yao kwenye Kitengo cha Usalama wa Moto. Wafanyakazi wanaweza kuwasiliana na Utawala wa Usalama wa Afya na kazini, wa Jimbo la Vermont (VOSHA) kwa 1-800-287-2765. Chukulia kuwa kuna ukungu nyumbani mwako ikiwa lilijaa maji na halikukaushwa vyema ndani ya masaa 24 hadi 48. Hakikisha kukausha nyumba yako kabisa baada ya mafuriko. Ukungu utarudi ikiwa jengo lako halijakauka kabisa. Tumia visafisha hewa vinavyo bebeka na vichujio vya HEPA wakati wa kusafisha, na tumia karatasi za plastiki kuzuia ukungu kuenea. Fungua madirisha na milango yote ili hewa ifuatie nje, na utumie feni na viondoa unyevu ili kuelekeza mwendo wa hewa. Tumia feni au shabeki pekee katika nafasi zilizo-dhibitiwa au ili zipeperushe hewa nje, au zisi-peperushe sehemu nyingine za nyumba yako. Fuata hatua tulizo zungumzia hapo awali ili kuondoa ukungu kutoka kwa nyumba yako. Huenda ukahitaji kuua vijidudu maeneo ambayo yamegusana na maji ya mafuriko ili kuondoa vijidudu. Video nyingine yenye mwongozo wa kusafisha nyumba yako kwa usalama itacheza baada ya video hii. Safisha nyuso za vitu vya ndani ukitumia sabuni na maji kwanza, kisha fuatilia na kuuwa vijidudu vilivyomo eneo hilo. Kumbuka, umuhimu wa kuzuia ukungu, ni kuweka nyumba yako au jengo lako liwe kavu. Kwa habari zaidi tembelea tovuti hii:

Comment