Watoto 46 wakiwemo 12 wa madarasa ya awali wanaolelewa katika Kituo Cha kulea watoto yatima na wanaoishi kwenye mazingira magumu Cha Buloma wamepatiwa misaada mbalimbali ya chakula kwa ajili ya kusherehekea sikukuu ya pasaka na kuwa na furaha kama wengine .
Msimamizi wa Kituo Cha Buloma Baraka Peter amesema kuwepo kwa idadi hiyo ya watoto inapelekea kuwepo Kwa mahitaji mengi Kila siku na hivyo msaada huo ni faraja kubwa Kwa watoto hao ambao nao wameishukuru kampuni ya uuzaji na usambazaji vifaa vya ujenzi na vyuma chakavu Kyem General Supplies Ltd ya mjini Kibaha Kwa kuwapatia chakula Cha Sikuu ya Pasaka