Ufugaji wa kuku chotara hatua kwa hatua
KUKU CHOTARA
Hawa ni aina ya kuku ambao wamechanganya aina fulani ya kuku na aina nyingine ya kuku na kupata aina moja ya kuku, mfano: amechukuliwa jogoo wa kienyeji akachanganywa na tetea wa kisasa na vifaranga vitakavyotoka vitakuwa chotara kwa maana watakuwa na sifa baadhi za kienyeji na sifa baadhi za kisasa.
Kuku hawa kwa hapa nchini wapo wengi na kuna makundi mbalimbali ya kuku kulingana na asili na mahali walipo tokea, mfano: MALAWI, KENBRO, SASSO na KROILA na hawa wanatofautiana sifa na asili.
Faida ya kuku chotara
Hapa nitataja kwa ujumla faida zote.
Wanakuwa kwa haraka na wanakuwa na maumbo makubwa tofauti na kuku wa kienyeji hivyo ni wazuri sana kwa nyama.
Ni watagaji wazuri sana tofauti na kuku wakienyeji (kuku hawa ukuwahudumia vizuri wanataga mayai kati ya 180-260 kwa mwaka hivyo ni wazuri sana kwa mayai.
Wanaishi kwenye mazingira yeyote yale kwa maana wanaweza kuishi vizuri wakiachiwa kujitafutia chakula.
Wanastahimili sana magonjwa (chanjo ni Muhimu kuwapa) tofauti na kuku wa nyama au wa mayai.
Nyama yao ni nzuri sana haina tofauti na kuku wakienyeji.
Wanauzito mkubwa kuku mmoja anafika hadi kg 4.5
Soko lake ni kubwa.