Joti a.k.a Lucas Lazaro Mhuvile ni msanii wa vichekesho, mshereheshaji na mzalishaji wa vipindi ya televisheni na redio nchini Tanzania. Joti amekuwa katika sanaa kwa zaidi ya miaka 20 na ni moja ya wasanii mahiri zaidi wa vichekesho kuwahi kutokea nchini Tanzania.