TUMESHUHUDIA wachawi wakiwatesa watu wasio na hatia hata kuanzisha vita na waganga wa jadi ambao hujitolea kuwasaidia waliowaroga kuwaondolea mateso mazito kutokana na kutupiwa uchawi ambao huwatesa katika maisha yao yote. Tumeshuhudia vifo vya ghafla vya watu na baadaye kusikika wameonekana sehemu fulani wakiwa hai au wamegeuzwa misukule.