MENU

Fun & Interesting

HOTUBA YA MHE. RAIS DKT. MAGUFULI BAADA YA KUWAAPISHA VIONGOZI IKULU JIJINI DSM - NOVEMBA 12, 2018.

Ikulu Tanzania 25,696 lượt xem 6 years ago
Video Not Working? Fix It Now

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 12 Novemba, 2018 ametangaza uamuzi wa Serikali kununua korosho zote za wakulima msimu huu kwa bei ya shilingi 3,300 kwa kilo baada ya wanunuzi binafsi kushindwa kutimiza maagizo ya Serikali kwa kuanza kununua kwa kusuasua na kwa bei isiyoridhisha.
Mhe. Rais Magufuli ametangaza uamuzi huo Ikulu Jijini Dar es Salaam muda mfupi baada ya kuwaapisha Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Joseph George Kakunda, Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Ngailonga Hasunga, Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Dkt. Mary Machuche Mwanjelwa, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Constantine John Kanyasu, Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Innocent Lugha Bashungwa, Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Mwita Mwikwabe Waitara na Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Mhe. Jaji Mstaafu January Henry Msoffe.

Comment