UFUGAJI WA KUKU CHOTARA KUROILER
Biashara ya ufugaji wa kuku chotara imegawanyika katika makundi tofautitofauti, makundi hayo ni kama yafatayo:-
1. Uzalishaji wa mayai au vifaranga au vyote kwa pamoja
2. Uzalishaji wa vifaranga wa wiki 4-5
3. Uzalishaji wa kuku chotara kwaajili ya nyama
Kabla haujaanza ufugaji wa kuku chotara yakupasa uwe umechagua ni aina gani ya bidhaa unataka kuingiza sokoni. Soko kubwa la kuku chotara ni wafugaji ambao wanataka kuingia kwenye biashara hiyo, kwahiyo yakupasa mhamasishaji na uwe na ushiwishi kwa wengine ili kujitanulia soko.
Jifunze Zaidi: https://youtu.be/NDdluGWDzys
Lakini zipo hatua ambazo inakubidi uzifahamu na uzipitie ili uweze kufuga kuku chotara kwa mafanikio.
Hatua hizo ni kama zifatazo:-
1. Unahitaji Kuzalisha Bidhaa ya aina gani .
Kama nilivyotangulia kusema hapo awali kuwa ufugaji wa kuku chotara umegawanyika katika makundi tofautitofauti, unapo hitaji kuanza ufugaji wa kuku chotara unatakiwa kuchagua kundi moja na ukawekeza nguvu ya kutosha ili kuongeza thamani ya utakachozalisha.
2. Kutafuta elimu ya ufugaji wa kuku chotara.
Elimu ya ufugaji wa kuku chotara ni muhimu sana na itakupa mwanga wa utakachenda kukifanya.
Elimu hiyo ihusishe vitu vifatavyo;-
I. Ujenzi wa Banda la kuku chotara
Katika vitu ambavyo mfugaji wa kuku chotara unanatakiwa kuvizingatia ni ujenzi wa banda la kuku kwa sababu hawa kuku chotara wanaathiriwa sana na hali ya hewa inayosababishwa na mazingira ukilinganisha na kuku wa kienyeji.
II. Utaratibu wa kuwapa chanjo vifaranga
Hili halina mjadala, ili kuwakinga kuku wako dhidi ya magonjwa yasiyokuwa na tiba na ambayo husababisha vifo kwa asilimia kubwa ni kuwa na elimu ya kuwapa chanjo kwa wakati.
III. Udhibiti wa Magonjwa mbalimbali yanayosababisha vifo kwa kuku, magonjwa haya ni magonjwa ya miripuko kama typhoid, kipindupindu, coccidiosis, Coryza n.k
IV. Jinsi ya kuwalisha kuku kwenye umri tofauti ili kuhakikisha wanakuwa vizuri na wanataga mayai mengi.
V. Mbinu za kupunguza gharama za ulishaji wa chakula, mfano kuwalisha hydroponics na Azolla n.k.
3. Fahamu bajeti ya uendeshaji wa mradi.
Fanya hesabu ya kila kitu kinachohitajika ili kufahamu bajeti ya uendesgaji wa mradi, kuanzia vifaranga wanaingia bandani mpaka kufikia uzalishaji. Hesabu hiyo ihusishe vitu vifatavyo:-
I. Gharama ya ujenzi wa banda
II. Vifaa muhimu bandani
Vyombo vya chakula na maji kwenye umri tofauti, vyanzo vya joto (jiko au balb), bruda, thermometer, mkaa, maranda na magazeti
III. Chakula kwa rika tofauti
Gharama ya chakula watakachokula mpaka waanze uzalishaji
IV. Chanjo na antibiotiki
Gharama ya antibiotiki na chanjo watakazotumia mpaka kufikia uzalishaji
V. Gharama ya umeme
4. Jenga Banda Bora.
Kama nilivyotangulia kusema hapo awali banda la kuku chotara linatakiwa likidhi vigezo ili liweze kuwalinda kuku wako dhidi ya magonjwa ya miripuko hasa typhoid, coccidiosis, Coryza na kipindupindu.
5. Ingiza vifaranga Bandani.
Hii ni hatua muhimu sana kwenye ufugaji wa kuku chotara na kama mfugaji unapaswa kuwa makini sana katika uchaguzi wa kampuni au wauzaji wa vifaranga.
Kunamadhara makubwa sana kama utanunua vifaranga kutoka kwa wauzaji wasio aminika kwa sababu ya magonjwa ya kurithi vizazi hadi vizazi au wauzaji wengine kukosa uaminifu na kukuuzia vifanga wasiokuwa chotara.
Kuna kesi nyingi nimewahi kuzipokea kutoka kwa wafugaji wa kuku chotara, wakilalamika kuchanganyiwa vifaranga wa aina tofautitofauti.
6. Ulishaji wa chakula na utoaji chanjo kwa vifaranga.
Katika kuhakikisha vifaranga wanakua na afya njema, chakula bora na chanjo ni vitu vya kuzingatia sana.
Jinsi ya kuwalisha vifaranga wako itategemea na kundi la ufugaji ulilolichagua kati ya makundi matatu niliyoyazungumzia hapo awali. Vifaranga wa kuku chotara wanatakiwa kulishwa kulingana na malengo ya mfugaji, anayehitaji kuwauza kwaajili ya nyama atawalisha tofauti na anayehitaji mayai ya kutotolesha vifanga kwahiyo tuzingatie hili.
7. Udhibiti wa Magonjwa ya Miripuko.
Magonjwa ya kuku yamegawanyika katika makundi tofautitofauti
I. Magonjwa yanayo sababishwa na virusi
Magonjwa haya yanachanjo na wafugaji wengi huwa wanazingatia na wanafanikiwa kuyadhibiti
II. Magonjwa yanayo sababishwa na bakteria
Magonjwa haya ndio tatizo kubwa kwa wafugaji kwa sababu vimelea vyake vimezagaa kila mahali na vinapatikana kwenye uchafu na unyevu
8. Soko
Kitu ambacho kinawatisha watu wengi kuingia kwenye ufugaji wa kuku chotara, ni stori zinazoendelea mtaani kuhusu soko la kuku chotara. Wengi wanasema soko la kuku chotara ni gumu, lakini sisi changamkia fursa tuasema soko la kuku chotara ni pana na la wazi. Yeyote anaweza akauza bidhaa anayozalisha. Ili uweze kuwanasa wateja wa bidhaa za kuku chotara, unatakiwa kuwa karibu na wafugaji wenzio, uwahamasishe wanaokatishwa tamaa kuhusu kuku chotara.