MENU

Fun & Interesting

Magonjwa ya Kuku wa Kienyeji na Jinsi ya Kutibu

Changamkia Fursa 71,170 lượt xem 3 years ago
Video Not Working? Fix It Now

Magonjwa ya Kuku wa Kienyeji ni changamoto kubwa kwenye ufugaji wa kuku ambayo huwakatisha tamaa Wafugaji wengi kwa sababu ya vifo vingi hasa kipindi cha uleaji wa vifaranga na hata kuku wakubwa.

Magonjwa yamegawanyika katika makundi mbalimbali kulingana na wadudu wanaosababisha magonjwa hayo.
Kuna magonjwa yanayo sababishwa na virusi, magonjwa yanayo sababishwa na bakteria, magonjwa yanayo sababishwa na protozoa, magonjwa ya upungufu wa lishe na magonjwa yanayosababishwa na wadudu (minyoo, viroboto na utitiri).

Bakteria wanaosababisha magonjwa ya kuku wa kienyeji
hupatikana kwenye miili ya kuku wagonjwa, utumbo, makamasi, na vinyesi vyao.
Aidha
katika mazingira machafu na vyakula, maji, hewa, na vifaa vya kazi vilivyo chafuliwa.
Mazingira yenye unyevunyevu na joto ni vichocheo vya kuzaliana na kusambaa kwa
bakteria.

Magonjwa ambayo yameelezewa kwenye video hii ni
1. Typhoid
2. Kipindupindu
3. Coccidiosis

Sasa kwakuwa magonjwa yote yamebainika kwenye banda moja sasa unapaswa kutumia dawa yenyeuwezo wa kutibu magonjwa yote, mfano wa dawa hiyo ni ESB3 30% n.k Au
Uchanganye dawa zifatazo Trisulmycine na Amprollium.

#magonjwayakukuwakienyeji

Comment